Wakati serikali inafanya jitihada za kutokomeza
magonywa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa
kipindupindu na magonjwa mengine ya tumbo
kwa kuhamasisha usafi na kutunza mazingira hali
iko tofauti katika kiwanda cha mafuta ya Alizeti
cha JIE-LONG cha mjini Shinyanga
kinachomilikiwa na mwekezaji kutoka China kwa
kuchafua mazingira na kutiririsha maji machafu
katika makazi ya watu hali inayosababisha mazao
ya wakulima kukauka na baadhi ya mifugo
kupoteza maisha kwa kunywa maji yenye
kemikali.
Akizungumza wakati wa ziara ya kushtukiza
katika kiwanda hicho mkuu wa wilaya ya
Shinyanga mjini Bi.Josephine Matito ametoa siku
saba kwa uongozi wa kiwanda hicho kuweka
mazingira katika hali ya usafi na kurekebisha
mfumo wa majitaka vinginevyo kiwanda
kitafungiwa huku akimtaka ofisa afya wa
halmashauri ya Shinyanga mjini kuliandikia barua
baraza la uhifadhi na utunzaji wa mazingira
(NEMC) kufika katika kiwanda hicho kukagua ili
kujiridhisha na hali halisi iliyopo kiwandani hapo.
Katika hatua nyingine Bi.Matiro ameuagiza
uongozi wa shirika la reli Tanzania (TRL) kituo
cha Shinyanga kufanya usafi na kufyeka msitu
wa majani uliopo katika eneo hilo kwakuwa
maeneo hayo yamekuwa maficho ya wezi na
vibaka nyakati za usiku huku baadhi ya watu
wakitumia fursa ya vichaka hivyo kufanya ngono
zembe nyakati za usiku hali inayotishia
kuongezeka kwa ugonjwa wa ukimwi
namagonjwa mengine ya zinaa huku mkuu wa
kituo cha reli cha Shinyanga Bw.Baruhani Issa
akikiri kuwepo kwa hali mbaya ya uchafuzi wa
mazingira katika eneo lake na kuahidi
kushirikiana na watumishi wenzake kutekeleza
agizo la mkuu wa wilaya.
Uncategories
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga atoa onyo
kwa kiwanda cha mafuta ya Alizeti
kinachomilikiwa na mchina.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon