Polisi wateketeza zaidi ya tani moja na nusu ya bangi Kibondo mkoani Kigoma.

Jeshi la Polisi wilayani Kibondo mkoani Kigoma
limeteketeza zaidi ya tani moja na nusu ya bangi
iliyokuwa imepandwa katika shamaba la ukubwa
wa hekari mbili katika kijiji cha Kagoti kata ya
Misezero wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Ruth Msafiri
amesema, walipata taarifa za kuwepo shamba la
bangi katika kijiji hicho hali iliyowalazimu kufika
kijijini hapo alfajiri na kufanya ukaguzi ambao
ulibaini shamba hilo likiwa limechanganywa na
mazao mengine na kwamba wataendelea
kuchukua hatua dhidi ya wananchi ambao
wameamua kulima bangi badala ya mazao
yanayokubalika.
Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya
Kibondo mkaguzi msaidizi wa polisi Maiko
Joshua amesema pamoja na bangi iliyokutwa
shambani, baada ya upekuzi katika nyumba ya
watuhumiwa wamekuta kilo moja ya bangi kavu
na kwamba watuhumiwa watafikishwa
mahakamani wiki hii.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post