VYETI VYA KIDATO CHA SITA NIUTATA SOMA

Baraza la Taifa la Mitihani (Necta),
limeagiza kusitishwa kwa ugawaji wa vyeti
vya kidato cha sita kwa wanafunzi
waliohitimu mwaka 2015, huku vile
vilivyokwisha gawanywa kwa watahiniwa hao
vikitakiwa kurejeshwa kwenye chombo
hicho.
Hali hiyo imeibua utata mkubwa, huku
baadhi ya wadau wakiwamo maofisa elimu,
wakihisi hatua hiyo ya Necta huenda
inalenga kuvibadili vyeti hivyo kutoka
kwenye mfumo wa wastani wa alama (GPA),
kwenda kwenye ule wa jumla (division).
Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Juma
Kaponda, alipoulizwa kama amepokea agizo
hilo, alithibitisha kuwa shule zote za mkoa
huo zenye kidato cha tano na sita zimepewa
taarifa ya kutakiwa kurudisha vyeti hivyo
Necta.
Alisema sababu ya kuvirudisha vyeti hivyo
anadhani ni kufanya mabadiliko kutoka GPA
na kurudi kwenye divisheni.
Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha, Nestory Mloka,
alisema amepata barua ya maelekezo hayo
kutoka Necta ikimuelekeza kuwataka
maofisa elimu wilaya wawasiliane na wakuu
wa shule za kidato cha tano na sita
wasigawe vyeti vya wanafunzi waliohitimu
mwaka 2015.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Matthew
iliyoko Kongowe, Mkuranga mkoani Pwani,
Abraham Shafuri, naye alikiri kuwapo kwa
agizo la Necta la kusimamisha utoaji wa
vyeti hivyo kwa wahusika.
Alisema aliambiwa na maofisa wa Necta
kuwa vyeti hivyo vinatakiwa kurejeshwa
kwenye baraza hilo na kwamba sababu
zilizotolewa ni kuwa kuna marekebisho
kidogo yanapaswa kufanyika.
“Nilichoambiwa ni kwamba shule karibu zote
za Dar es Salaam zimesharejesha vyeti hivyo
na kwamba kwa sisi wa mkoa wa Pwani,
maofisa hao watapita kuvichukua lakini hatujui
ni lini watakuja,” alisema Shafuri.
Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk,
Charles Msonde, alipoulizwa alikanusha
vikali madai hayo, akisema vyeti hivyo
havitabadilishwa kutoka kwenye mfumo
wake bali vimesitishwa kugawanywa ili
baraza lijiridhishe na baadhi ya vitu.
“Vyeti hivi baraza limevigawa hivi karibuni na
lilichofanya sasa limezuia kwanza shule
zisigawe mpaka litakapotoa maelekezo
mengine, msingi huo wa kuzuia uko kwenye
hoja ya kuhakikisha tu kwamba linajiridhisha
kwenye takwimu zake kama zimekaa sawasawa
katika vyeti vilivyokwenda kila shule.
“Baadhi ya vyeti kwenye mkoa wa Dar es
Salaam vipo Necta, lakini kwenye mikoa
mingine yote viko shuleni,” alisema Dk
Msonde na kuongeza;
“Kama mkuu wa shule alikuwa amegawa vyeti
viwili, vitatu kabla havijarejeshwa baraza ni
suala jingine, lakini kiujumla kinachofanywa na
baraza hapa ni kuhakiki cheti hiki, kama
vimekaa kama utaratibu wetu ulivyo.”
Alisema suala la kubadilisha kutoka kwenye
GPA kwenda kwenye divisheni halipo na
kwamba matokeo yaliyotangazwa kwa
utaratibu wa GPA vyeti vyake vitaendelea
kuwa katika mfumo wa GPA na matokeo
yaliyotangazwa kwenye utaratibu wa
divisheni vyeti vyake vitabaki kuwa kwenye
divisheni.
Alisema kwa wale ambao tayari wako nje ya
nchi, hakuna atakayeathirika na kama
baraza likihitaji cheti chake litafanya
utaratibu wa kukipata.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post