PRODUCER SCOTT STORCH WA MAREKANI AMEMSHAMBULIA MKALI LAMAR INSTAGRAM, KISA?

Producer maarufu kutoka Marekani Scott Storch,
aliyetengeneza hits za mastaa kadhaa
wakiwamo Rick Ross na Chris Brown,
amemshambulia mtayarishaji wa muziki kutoka
studio za Fishcrab Tanzania, Lamar kisa kapost
kipande cha beat yake.
Ilikuwa majira ya usiku wa jana Lamar alipost
clip ya beat hiyo ya Scott na kumtag kama
miongoni mwa watu wanaomuhamasisha kikazi.
Scott alionesha ghadhabu na kucoment kwenye
post hiyo akimuuliza Lamar kwanini anapost
beat yake?. Lamar alimueleza vizuri tu kuwa
anahamasika na kazi za Scott na anamuangalia
kama watu anaofata nyendo zao.
Mmarekani huyo akamtaka Lamar aache
kufanya hivyo ambapo alijibiwa ‘sawa kaka’.
Watanzania kadhaa wakiwamo wasanii Julio
Batalia, Dogo Janja na Lucci wamemshukia
Scott kwa kutothamini heshima anayopewa na
maproducer wanaochipukia.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post