NIVA: NIMESHAMSAIDIA SANA PESA NAY WA MITEGO, NA WATU TUNAOMJUA VIZURI HATUBABAISHI TUNAMFAHAMU KWA JINA LA ‘IMA CHOGO’.

Msanii wa Filamu Bongo, Niva super Mario,
amesema anamshangaa mwanamuziki Nay wa
Mitego kumrushia vijembe kwenye nyimbo zake
wakati yeye amemsaidia mambo mengi ya
kimaisha rapa huyo.
Akizungumza kupitia kipindi cha Twenzetu cha
Times fm, Niva amedai mara kadhaa Nay
alikuwa akikwama kipesa na yeye anaingia
gharama kumsaidia.
“Sikia niseme jambo, nimehama nyumbani 2010
nikaenda kupanga Sinza Mori, Nay amekuja
kwangu mwaka 2012 kaibiwa kila kitu kwenye
gari yake nikamsaidia tukafurahia kwangu ili
apooze machungu, sasa kama sina pakukaa pale
alikuja kwa nani??.
Sio hilo tu wakati tupo kwenye kampeni Nay
alivamiwa kwake Dar akawa anataka msaada
wa pesa nikatoa kumkabidhi milioni 2.5, na ndio
kipindi ambacho Shamsa alimpa kibuti, aliachwa
na shamsa kwenye Tour za kampeni Mwanza
sababu hajielewi” Alisema Niva.
Katika Line nyingine mkali huyo aliyetamba na
filamu ya Mario, amedai amemfahamu Nay kwa
mika kadhaa wala hababaishwi na chochote,
huku akiongeza kuwa yeye anamfahamu rapa
kwa jina la ‘Ima chogo'” alimaliza.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post