Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli
Tanzania (TRL), Kipallo Kisamfu na wenzake 10
wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu wakikabiliwa na mashiataka tisa yakiwemo
ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kupitisha
ununuzi wa mabehewa mabovu 25.
Watuhumiwa hao pia kwa mujibu wa hati ya
mashitaka wanadaiwa kupitisha malipo ya zaidi
ya shilingi bilioni 2.8 kinyume na taratibu.
Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao
mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Emmilius
Mchauru. Huku upande wa jamhuri uoliongozwa
na mawakili wa serikali waandamizi, Shadrack
Kimaro, Theophil Mutakyawa na waendesha
mashitaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa (Takukuru), Max Ally na Maghela
Ndimbo.
Max alidai katika shitaka la kwanza, kati ya
februari mosi, 2013 na juni 30, 2014 makao
makuu ya TRL, mshtakiwa Kisamfu akiwa
mkurugenzi mtendaji kwa nia ovu alitumia vibaya
nafasi yake kwa kushindwa kusimamia zabuni na
kusababisha kampuni ya M/S Hindusthan
Engineering and Industries Limited kupata faida.
Shitaka la pili linamkabili mshtakiwa wa sita,
Mafikiri, ambaye ilidaiwa kuwa kati ya julai mosi
na agosti 31, mwaka 2013, makao makuu ya TRL,
akiwa fundi mkuu, alitumia vibaya madaraka yake
kwa kupitisha ramani ya mabehewa iliyoandaliwa
kinyume cha sheria na kuisababishia kampuni ya
m/s hindusthan engineering and industries
limited kupata faida.
Max aliendelea kudai kuwa kati ya januari mosi
na februari 28, mwaka 2014 makao makuu ya
TRL, akiwa kaimu mkuu wa ufundi, aliidhinisha
kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industries Limited kufanya ukarabati wa
mabehewa 25 bila kujiridhisha na maombi ya
tenda hiyo.
Katika shitaka jingine, ilidaiwa kuwa kati ya
januari mosi na februari 28, mwaka 2013, TRL,
mshtakiwa wa nne, saba, nane, tisa na 10,
wakiwa wajumbe wa kamati ya kutathmini zabuni
walitumia madaraka yao vibaya kwa kupitisha
kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industries Limited kufanya ukarabati huo na
kuisbabishia kupata faida.
Washtakiwa walikana mashitaka yao. Upande wa
jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika na haukuwa na pingamizi la
dhamana.
Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza, tatu, nne na
wa 11 walitimiza masharti hayo na kesi hiyo
itatajwa februari 25, mwaka huu.
Washtakiwawaliopandishwa kizimbani ni pamoja
na Jasper Kisiraga, Mathias Massae, Muungano
Kaupunda, Ngoso Ngosomwiles, Paschal Mafikiri,
Kedmon Mapunda, Felix Kashaigili, Lowland
Simtengu, Joseph Syaizyagi na Charles Ndenge.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon