Rais Magufuri Asema

Tanzania haiwezi kwenda mbele bila kuwa na
fedha zake, wafanyabiashara wanakwepa sana
kodi. Tunataka fedha tunazozikusanya ziende
kuwasaidia watanzania wa hali ya chini.
Zipo kejeli nyingi kuwa ni nguvu ya soda, hata
kama ni soda ukiweka gongo utalewa, kwa hio hii
ni soda special.
Tumeweka bilioni 200 kwa ajili ya daraja la Coco
beach hadi Agha Khan, barabara ya kutoka Rangi
tatu pia tumeitengea fedha na interchange ya
ghorofa tatu pale Ubunge
Shirika la ndege tunataka kulifufua ndio maana
tunachukua hatua mbalimbali. Yuko mmoja
ameshikwa pale alikuwa anataka kubadilisha
fedha kwenye akaunti tukamkamata, hatutaki
kusema mengi kwa sababu hatua zinachukuliwa
ikiwemo za kimahakama.
Watanzania tujifunze kulipa kodi, chochote
unachoenda kununua omba risiti. Kuna sehemu
inatakiwa kubaki kwa ajili ya kuhudumia watu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post