Mkandarasi akamatwa na polisi kwa kushindwa kulipa vibarua wilayani Ukerewe.

Mkandarasi wa kampuni ya Nyakarungu CIVIL
CONSTRUCTION, Harrison Odila ametiwa nguvuni
na jeshi la polisi mjini Nansio wilayani Ukerewe
kwa madai ya kushindwa kuwalipa vibarua zaidi
ya 100 waliokuwa wanajenga barabara ya Butiriti
– Guguyu yenye urefu wa kilometa tano kwa
kiwango cha udongo.
Mkandarasi huyo amekamatwa na askari polisi
wa kituo cha Nansio akiwa katika ofisi za makao
makuu ya halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, saa
chache baada ya vibarua hao kufanya
maandamano ya kudai malipo yao kiasi cha
shilingi milioni moja laki mbili na elfu hamsini.
Diwani wa kata ya ngoma ambako barabara hiyo
imejengwa na kukamilika tangu mwezi Septemba
Mwaka jana Bw.Msingi Musese amelalamikia
kitendo kilichofanywa na mkandarasi huyo cha
kuwapiga danadana vibarua hao.
Mkuu wa idara ya ujenzi katika halmashauri ya
wilaya ya Ukerewe mhandisi mapinduzi Magesa
Mwita ambaye ameshuhudia mkandarasi wa
kampuni hiyo ya nyakarungu akitiwa nguvuni na
askari polisi wawili alikuwa na haya ya kusema
kuhusiana na wakandarasi wenye tabia kama
hiyo.
Haya ndiyo majibu ya mkandarasi huyo,Harrison
Odila katika mahojiano baada ya kukutana
na vibarua hao ofisi za halmashauri ya wilaya ya
Ukerewe.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post