Ujambazi Mbagala watu saba wameuawa akiwemo askari polisi mmoja,askari binafsi wawili na raia jijini Dar es Salaam.

Watu saba wakiwemo majambazi watatu
wameuawa baada ya kutokea kurushiana risasi
kati ya majambazi na Polisi kabla na baada ya
majambazi hao kuvamia tawi la Access Benki
lililopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi katika kanda maalum ya dar
es salaam kamishina simon siro amesema
majambazi 12 wakiwa katika pikipiki sita
walivamia benki hiyo kwa nia ya kuiba fedha
jaribio ambalo kwa kiasi kikubwa halikufanikiwa.
Amesema mbali ya majambazi watatu
kuuawa,pia Polisi mmoja,askari wa kampuni
binafsi ya ulinzi na raia wawili nao waliuawa
katika tukio hilo ambapo majambazi
walizitelekeza pikipiki zao na kuchanganyika na
raia na baadaye kudaiwa wamekimbilia katika
msitu wa Kongowe unaotenganisha mkoa wa
DSM na Pwani.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles
Kitwanga amesema mara baada ya mkutano huo
na waandishi wa habari atawasiliana na waziri
wa ulinzi ili wapatikane askari kutoka JWTZ
kusaidia msako wa majambazi ambao
wanadaiwa kujificha katika misitu
inayotenganisha mikoa hiyo miwili.
Nao waendesha pikipiki wametakiwa kuwa
wavumilivu kwani kuanzia sasa msako maalum
unaendelea kuwabaini wahalifu ambao wengi
wao hutumia Pikipiki.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post