Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu
amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda
wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul
amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na
Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich
Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo
Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa
Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa
Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa
Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi
ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana
Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi
mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi
amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi
inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi
mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.
Aidha,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius
Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi
yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao
Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. Aliyekuwa
Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda
kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi
aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar
es Salaam.
Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi
DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao
Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa
Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja
na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine
Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa
Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.
› IGP Mangu afanya mabadiliko ya
makamanda wa polisi kwa baadhi ya Mikoa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon