TUMISHI ZA KUZUIA WIZI WA SIMU ZA KISASA ZILIZOTENGENEZWA KWA MFUMO WA ANDROID

Unaweza kufanya vitu vingi vya maana
kwa kutumia simu yako
iliyotengenezwa kwa mfumo wa
Android mbali na kupiga,kupokea
simu,huduma ya ujumbe mfupi wa simu
na intaneti.
Mojawapo ya mambo ya kuvutia katika
simu za Android ni kuitumia kuwa na
mfumo wa mlio wa kuzuia wezi,kama
ilivyo katika simu za iphone ambayo
hutumia program tumishi ya Find My
Iphone.
Kuna program tumishi nyingi ikiwemo
ya Google iitwayo Android Discovery
Manager ambayo inafanya kazi kwa
watumiaji wa simu walio na barua
pepe za google ambayo huwezesha
kufahamu eneo ilipo simu yako.
Pia kuna program tumishi ambayo
huwezesha simu yako kutoa mlio iwapo
mtu atahamisha simu yako mahali
ilipo,nyingine ni ile inayopiga
picha kwa camera ya mbele kwa mtu
atakayejaribu kufungua simu yako kwa
kuuingiza neno la siri la uongo.
Kuna program tumishi iitwayo Anti
Theft Alarm inayopataika katika
Google Play Store ambao inazuia
simu yako ya Android katika aina
mbalimbali za wizi.Program hii
tumishi ya kuzuia uhalifu na
inaelezwa kuwa ni miongoni mwa
program tumishi bora za kuzuia wizi
wa mitandao ambapo mtu anaweza
kutumia kuzuia wizi wa komputa
mpakato,nyaraka,barua pepe n.k
ambapo nayo huwezesha simu kutoa
mlio mtu anapoihamisha ilipowekwa

Previous
Next Post »

Ads Inside Post