Man united Felipe Anderson kusajiliwa Man United leo Feb 22 kwa euro milioni 60, huu ndio ukweli wenyewe

February 22 vyombo kadha vya habari viliripoti kwa kuandika  stori kuwa klabu ya Man United imefanya usajili wa kiungo mshambuliaji wa Lazio  Felipe Anderson. Taarifa hiyo ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii inaeleza kuwa Man United na Lazio wamekubaliana kila kitu kuhusu usajili wa kiungo na kuwa anasubiri kujiunga na Man United mwisho wa msimu.

 Felipe Anderson aliripotiwa kuwa usajili wake wa kujiunga na Man United mwisho wa msimu umekalishwa kwa dauli la euro milioni 60, stori zilianza kuandikwa zaidi mchana wa February 22, lakini jioni ya February 22 Rais wa klabu ya Lazio Claudio Lotito amekanusha stori hizo na kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliofanyika kati ya Man United na Lazio.

Kiungo wa kimataifa wa Brazil Felipe Anderson ambae ndio alikuwa anatajwa kuwa atajiunga na Man United mwisho wa msimu, aliwahi kutamba na klabu ya Santos kabla ya kutua Lazio ya Italia mwaka 2013 na amecheza zaidi ya mechi 60.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post