KWENDA LOLLIPOP
No Computer needed…..
Utangulizi:
Bado Teknologia inakua kila sekunde.. Yapo
Maboresho kila Nyanja hasa katika Mawasiliano
kwa ujumla. Kompyuta na Simu za Mikononi
zimechukua nafasi kubwa katika Nyanja nzima
ya Mawasiliano.
Kampuni mbalimbali zakutengeneza simu nazo
kila nyakati zinajitahidi kutoa Matoleo mapya na
yalioboreshwa. Ipo mifumo (Operating Systems)
mitatu inayofanya kazi katika Simu za kisasa
zijulikanazo kama ‘Smartphones’. Mifumo ni
Android, iOS na Windows phone. Upo ushindani
mkubwa kwa Watengenezaji wake hali
inayosababisha Uboreshaji kwa kila mfumo.
Binafsi napenda mifumo yote lakini mfumo wa
Android ndio unatumika na watu wengi duniani
kwa sababu kuu zifuatazo;
(i) Simu zinazotumia mfumo huu zinauzwa kwa
Grarama ndogo zikilinganishwa na zinazotumia
iOS na Windows phone.
(ii) Kuna zaidi ya Program 1.6 million
zinazofanya kazi kwenye mfumo huu amabazo
mtumiaji anaweza kuzitumia kwenye simu
Yake kuendana na Mahitaji yake.
(iii) Ni rahisi sana ku root Simu za Android.
Rooting ni kitendo cha kukupa uwezo wa
kutumia na kuifurahia simu yako kwa
asilimia mia moja. Ukisha root simu yako
unakua na uwezo wa ku UPDATE mfumo wa
simu yako (Mfano kutoka Kitkat
kwenda Lollipop), kuweka Program zilizozuiwa
na Android Developers (Mfano program maalum
za Kutunza Chaji, ku ‘boost’
simu yako, kukuongezea RAM, program za
kukuwezesha kuipata simu yako hata pale mwizi
anapoi flash), kutoa ‘System
applications’ ambazo huna kazi nazo, kuufanya
mfumo wa simu UWE KAMA UTAKAVYO wewe,
nk…
Kwa waliobahatika kuisoma Makala yangu ya
JINSI YA KU ROOT SIMU YAKO YA ANDROID,
nafikiri wananielewa zaidi hapa.
Kawa hujaiona Tembelea ukurasa wangu wa
Facebook au wasiliana nasi 0766 598830
Waweza pia kui search google
Kwani iliwekwa kwenye tovuti ya JamiiForums.
(iv) Zipo Program/Applications nyingi na za
kisasa ambazo bado watumiaji wa iOS na
Windows phone hawajazipata.
Mfumo huu wa Android una Matoleo yafuatayo
hadi Makala hii inapoandikwa ambayo ni:
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
11. Marshmallow (6.0 --- )
Matoleo haya yanaboreshwa kila yajapo Mapya
na Mpaka ninapoandika Makata hii Simu nyingi
za Android zinazotumiwa na wengi zinatumia
Andriod 4.4 – 4.4.4 (Kitkat). Mfumo wa mwisho
(Marshmallow) umewekwa kwenye simu
zilizotolewa hivi karibuni kama vile Nexus 6P,
Nexus 5X nk... Kujua toleo lako nenda
Settings˃About phone˃Android version. Kama
upo Kitkat, huu ni Muda sahihi wa kufurahia
Lollipop Experience. Binafsi Simu yangu ni
Tecno H6 na nilishawishika kutoka KitKat
kwenda Lollipop kwa sababu zifuatazo:
(i) Mfumo wa Lollipop uko ‘stable’ na fasta
kuliko KitKat
(ii) Unatunza chaji kuliko Kitkat kwani ‘bugs’
nyingi zimekua fixed na pia ‘Power saving
feature’ imeboreshwa
(iii) Una mwanga zaidi (More brighter) na pia
una Visual effects nzuri na za kuvutia
(iv) Rahisi sana ku root
(v) Una uwezo wa ku manage app nyingi bila
ujumbe wa ‘program not responding’ au
‘Unfortunately, program has
stopped’
JINSI YA KU UPDATE KITKAT KWENDA
LOLLIPOP;
Vinavyohitajika;
- Muda
- Simu ya Android iliokua ROOTED tayari (ipo
Makala jinsi ya kuroot, kwa atakaehitaji)
- Memory Card isiyo na tatizo ( angalao 8GB)
- Kifurushi cha Internet angalao GB 1 (kwa ajili
ya ku download ROM na ku install program zako
muhimu baada ya kufanikisha
zoezi zima)
Zoezi hili ni LA HATARI SANA KWA
ATAKESHINDWA kufuata hatua zifuatazo kwa
MAKINI kwani Simu yako HAITAWAKA tena
ukikosea! Kinachotakiwa ni UMAKINI na Uhakika
wa USAHIHI kwa kila unachokifanya! Ndio
maana nimetangulia kusema andaa MUDA
maalum unapoanza—usiwe na kazi nyingine.
Binafsi nilisha update SIMU ZAIDI YA 40 sasa
bila kuua hata moja!
Kwa kuanza, naamini simu yako tayari umeshai
root, na sasa tuanze kupitia hatua moja baada
ya nyingine kufanikisha zoezi zima.
1. Hakikisha simu yako ina Chaji ya kutosha.
Inashauriwa wakati wa ku update iwe kwenye
chaji.
2. Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu
yako. Nenda Settings>About phone>Build
number. Baadhi ya simu (LG na
HTC) nenda Settings>About phone>Software
information>Build number. Ukishafika kwenye
Build number gusa hapo
mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You
are now a Developer” Sasa nenda
Settings>Developer options>USB
debugging. Weka tiki hapo (kama haipo). Hatua
hii kwa wengi hua ni tayari kwani hufanywa
wakati wa ku root.
3. Nenda settings>Security>Unknown Sources.
Weka tiki hapo (Kama haipo).
4. Nenda Playstore install program inayoitwa
[ROOT] Rashr – Flash Tool. Usiifungue baada
ya kui Install.
5. Hatua hii ni ya Muhimu sana. Kabla
hatujaiangalia tunapaswa kujua Mambo
machache.
(i) Recovery – Hiki ni kipengele cha Mfumo wa
simu au hata Computer ambacho
kimetenganishwa na Mfumo wa kawaida
Wa simu. Hiki husaidia tunapo flash/ku update
simu.
(ii) Bootloader ni sehemu ya Mfumo wa simu na
hata Computer ambacho ndicho huamua Simu
au Computer kuwakia
Kwenye Recovery au iwake kawaida. Kwa wale
wanao Install Windows OS kwenye Computer
zao wananielewa zaidi
hapa. Unapoweka DVD ya Windows files na
kuwasha PC yako na Kubonyeza F11 KEY. Hapo
ni kwamba unai Instruct PC
yako iwake kwenda kwenye Recovery. Ndicho
tunachokifanya tunapo Install Android Lollipop
ROM.
(iii) ROM (Operating System Image) – ni Flash
files ambazo ndizo huwekwa kwenya Read Only
Memory (ROM) ili simu
iweze kuwaka.
(iv) Android Custom Recovery. Watengenezaji
wa Simu za Android wame lock Bootloader ili
watumiaji wake wasiweze ku
Install ROMs mbalimbali kwenye simu hizo.
Wameweka Recovery ambayo hairuhusu kuflash
chochote.
Sasa hapa ndipo hatua ya tano ilipo, Ku Unlock
Bootloader ili tuweze ku flash ROM yoyote
kwenye simu ya
Android. Kufanikisha hatua hii tuna flash
Android Custom Recovery nyingine
itakayoturuhusu kuflashia ROM
mpya Kwenda kwenya Mfumo wa simu. Zipo
Android Custom Recovery mbili (2) ambazo
hutumika sana tunapo flash
Android Devices ambazo ni ClockworkMod
Recovery (CWM) na Team Win Recovery Project
(TWRP). Hapa nashauri twrp
kwani ni rahisi kutumia, inaeleweka zaidi na ina
Option nyingi.
Hatua za ku Install twrp;
- Kwa kutumia simu yako au PC, nenda google
kisha search tmrp ya Simu yako. Mfano kama
unatumia Tecno H6, search
‘twrp image for Tecno H6’ au ‘Team Work
Recovery Project image for Tecno H6’ kisha i
download.
- Ukishai download iweke kwenye Memory Card
ya simu unayotaka kuiflash.
- Fungua Rashr (rejea hatua ya nne hapo juu)
kisha gusa ‘Recovery from Storage’. Hapo
chagua twrp ulioi download.
Gusa ‘Yes’ utakachoulizwa. Kama itakua
imefanikiwa Utaona ‘ Partition flashed. Reboot
into Recovery now?’ Gusa ‘NO’
Kisha nenda hatua ya 6.
6. Hatua hii ni ya KU DOWNLOAD Lollipop ROM
kwa ajili ya SIMU YAKO. Ziko ROMs nyingi
kutoka kwa Developers tofauti.
Binafsi nilishakutana nazo nyingi na asilimia
kubwa zilikubali lakini nyingine hua zinakataa!!
Nenda Google kisha search ROM
ya Simu yako…Mfano kama unatumia Tecno H6;
search ‘Lollipop ROM for Tecno H6’ Nyingi hua
ni zaidi ya MB 200.
Tahadhari; Kabla ya ku download ROM
utakayoiona soma kwanza COMMENTS za
walioitumia ili uweze kujua kama ilikubali
kwao. Baadhi ya ROMs hua zilishakua infected
na Virus na ukizi Install hua zinakataa!! Na
zikikataa hua nia HATARI
kubwa kwani simu haitawaka tena!
Baada ya kui download iweke kwenye Memory
Card ya Simu unayotaka kui flash/update.
7. Hatua hii ndio kiini cha Zoezi zima! Nunua
kikombe cha Kahawa weka pembeni, mwombe
Mungu kisha ENDELEA….
Fungua tena Rashr kisha gusa ‘Reboot
Recovery’. Sasa simu yako itawakia kwenye
Recovery ( Team Win Recovery Project)
kama inavyoonekana pichani.
Kama tulivyokwishaona, zoezi la Kuflash
linaweza ku fail..na ikitokea SIMU HAITAWAKA
TENA!
Ni mpaka Computer na USB vitumike KUFUFUA
simu hio! Sasa kuepuka hili, hua tunahifadhi
mfumo uliopo ili likitokea tatizo
tuurudishe simu iwake.. Ili kuuhifadhi mfumo
uliopo, gusa ‘Backup’ , weka alama kwenye
Boot, Unboot, nvram, System,
na Cache,,, gusa Storage na uweke alama
kwenye sd card kisha ‘Swipe to Back Up’
Ikishamaliza ku back up rudi nyuma kisha gusa
‘wipe’ ˃ ‘Advanced wipe’ kisha weka alama
kwenye Dalvic Cache,
System, Cache na Data kisha ‘Swipe to Wipe’
Kumbuka ku format System ndicho kinachofanya
Simu isiwake tena kwani OS
haipo tena mpaka hatua hii. Kwa hio hakikisha
Backing Up Process ilikamilika kabla ya ku
format/wipe Simu.
8. Baada ya ku back up na ku wipe, rudi nyuma,
gusha ‘Install’, chagua ile ROM ya Simu yako
uliokwishai download kisha
‘Swipe to Confirm Flash’. Ni ndani ya Dakika
zisizozidi 10, utakua tayari una Android Lollipop
experience kwenye simu yako!!!
Gusa Reboot ˃ System
Angalizo; Kuna baadhi ya Lollipop ROMs
ambazo System apps hazijawa included. Uwe
makini hapo, kama hio ROM haina apps, lazima
kuna maelekezo ya ziada ulipoipatia hio ROM.
9. (Hatua hii ni endapo Flashing process ili
fail…) Gusa Restore, chagua Package yenye
tarehe sahihi kisha Swipe to Restore.
Hapo ule Mfumo uliopo utarudishwa na simu
yako ITAWAKA kama kawaida. Kama bado
utakua na nia Tafuta ROM nyingine tofauti kisha
jaribu tena.
Hitimisho:
Mwandishi wa Makala hii hatahusika kwa
Uharibifu wowote utakaofanywa na baadhi ya
Watu watakaokosa Umakini wakati wa Kuflash
Simu zao. Hatua zote zilizoelezewa hapa ni
SAHIHI na alieziandika hua anazitumia na
kufanikiwa.
Waweza pata Msaada kutoka kwa Mwandishi wa
Makala hii kama vile;
- Kupata ROM sahihi kwa ajili ya simu yako
(ndani ya saa 24). Hua nina ROM za simu
ambazo ni popular na zilikubali kwenye Simu
hizo. Ukihitaji utatumiwa ‘download link’ ili ui
download kwenye simu yako.
- Kua na mawasiliano ya moja kwa moja na
Mtaalam pale unapoanza zoezi hili… hapa
utakua unatoa taarifa kwa kila hatua ambayo
utakua huelewi au kama kuna tatizo.
- Kuuliza swali lolote kuhusu Makala hii.
Nikutakie kila la Kheri wewe utakaeamua
kuchukua hatua za kufurahia Maisha MAPYA na
Android Lollipop Experience…
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon