Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani
Shinyanga imeufunga mgodi wa uchimbaji wa
alimasi wa Elly Hilali ulioko Mwadui Shinyanga
kwa muda usiojulikana kwa kosa la kushindwa
kulipa deni la mapato ya serikali zaidi ya shilingi
milioni miatatu sabini na nne na laki tisa na
sabini huku wafanyakazi wa mgodi huo
wakilalamika kuathiriwa na kitendo hicho.
Akizungumza na Mwandishi kuhusu sakata la kufunga
mgodi huo wakala wa ukusanyaji mapato wa TRA
Bw.Lyasuka Ibrahim amedai TRA imelazimika
kuufunga mgodi wa almasi wa Elly Hilali hadi
kiasi cha deni linalodaiwa litakapolipwa huku
akidai kuwa uongozi wa mgodi umekaidi amri
halali ya kusitisha kazi zote mgodini hapo lakini
chakushangaza maofisa ukaguzi wa TRA
walipofika katika eneo hilo siku moja baada ya
kuufunga mgodi walikuta baadhi ya kazi
zikiendelea kama kawaida kinyume na maagizo
yao.
Naye kaimu meneja wa kitengo cha uzalishaji
katika mgodi huo Bw.Bader Seiph alipoulizwa
kwanini amekiuka amri ya kusitisha uzalishaji na
kuruhusu magari kuendelea kusomba kifusi
chenye madini ya alimasi alikataa na kudai
hakuna kazi inazoendelea mahali hapo lakini
maofisa wa TRA walipofuatilia walikuta magari
sita yakiendelea kufanya kazi na kulazimika
kuyakamata na kuyapeleka katika yadi ya TRA
iliyopo mjini Shinyanga kwa hatua zingine zaidi.
Nao baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo
wamelalamika kuhusu kufungwa kwa mgodi na
kuuomba uongozi wa mgodi kulipa deni hilo
mapema iwezekanavyo kwakuwa hali hiyo
itawafanya kuishi maisha ya shida huku meneja
wa TRA tawi la Shinyanga Bw.Ernesti Dundee
akidai kuwa zoezi la kuwasaka wakwepa kodi ni
endelevu hivyo makampuni mengine yalipe kodi
ya serikali kabla hayajafikiwa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon