Jeshi la Polisi mkoani Kagera limelazimika
kutumia nguvu katika kuwatawanya baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya CHICCO
toka nchini China inayojenga barabara ya
kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita
hamsini na tisa toka Kyaka hadi Bugene ambao
ni miongoni mwa wafanyakazi zaidi ya mia tano
wanaoidai kampuni hiyo zaidi ya shilingi bilioni
moja.
Mkuu wa jeshi la polisi wa wilaya ya Karagwe
Miki Makanja akitoa onyo kabla ya jeshi hilo
kuwatawanya wafanyakazi hao kwa mabomu na
maji ya kuwasha waliokuwa wakifanya
maandamano kuelekea kwenye ofisi za kampuni
hiyo kudai haki yao aliwaambia warudi
majumbani mwao au warudi kwenye maeneo ya
kazi kwa kuwa madai yao yanashughulikiwa na
ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kauli iliyopigwa
vikali.
Nao baadhi ya wafanyakazi walioongea na ITV
wakati wakielezea sababu za kufanya
maandamamo wameyataja madai yao ya tangu
mwaka 2013 ambayo hayajalipwa na kampuni ya
ukandarasi ya CHICCO kuwa ni pamoja na
mapunjo ya mishahara, fedha za kuachishwa
kazi, fedha za muda wa kazi ya ziada na fedha
za likizo, pia wamelalamikia vitendo ambavyo
hufanyiwa vya unyayasaji pale wanapodai haki
yao ambavyo wamevitaja kuwa ni kuachishwa
kazi bila sababu.
Kufuatia vurugu hizo meneja wa kampuni ya
CHICCO aliamua kujificha na hakutaka kuongea
na ITV iliyokuwa kwenye eneo la tukio, hata hivyo
ITV ilifanikiwa kumpata mwakilishi wa kampuni
ya TECU inayosimamia mradi wa ujenzi wa
barabara hiyo, mhandisi Mashubila Kamuhabwa,
akizungumza amesema ya madai ya wafanyakazi
hao kuwa ni halali na yanashughulikiwa,
amesema kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa
kulipa madai ya wafanyakazi hao wakati wowote
kuanzia sasa.
Uncategories
Polisi wawatawanya wafanyakazi wa
kampuni ya Chicco walioandamana wakidai
haki yao Kagera.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon