Tecno Phantom 5 ni simu nyingine ya kiwango cha juu kutoka kampuni ya Tecno

Kwa kipindi cha miezi kadhaa wengi
wametuomba tuichambue simu ya Tecno
Phantom 5, na tukataka tukifanya hivyo basi
iwe ni baada ya kuitumia. Ifahamu kwa
undani.
Tecno Phantom 5 ni simu nyingine ya kiwango
cha juu kutoka kampuni ya Tecno. Simu hii
ambayo imeanza kupatikana kuanzia miezi ya
tisa na kumi mwaka jana bado ni moja
inayoendelea kutangazwa sana na kampuni
hiyo hadi mwaka huu.
Je unapata nini pale unapoinunua?
Uwekaji wa simu kwenye boksi pamoja na
upangaji wa kisasa bado unaendelezwa na
Tecno. Kwenye boksi lake simu hiyo inakuja
na ‘cover’ lake, pia earphone pamoja na chaja
yake.
Kwenye boksi utapata chaja, earphone,
pamoja na cover.
Tazama video kutoka akaunti yetu ya YouTube
inayokuonesha utakachokutana nacho
ukifungua boksi la Tecno Phantom 5 mara
baada ya kununua.
Muonekano wa Tecno Phantom 5
Tecno Phantom 5 inakuja na kioo cha ukubwa
wa inchi 5.5 , kioo kikiwa ni cha teknolojia ya
vioo vigumu vya Gorilla Glass toleo la 3. Hii
ina maanisha kioo hakitachubuka au
kukwanguka kirahisi, ni kigumu kuvunjika pia.
Cha kusifiwa kwa Tecno kwenye Phantom 5 ni
pamoja na uamuzi wa kutumia chuma (Metal)
katika simu hiyo. Hii inaleta utofauti
ikilinganishwa na simu zingine ambazo
majumba yake (housing)
Inakuja na kamera mbili, ya selfi ni ya
megapixel 8 na inakuja na uwezo wa flash pia,
wakati kamera ya nyuma ni ya megapixel 13.
Nyuma pia kuna sensor spesheli ya kusoma
alama za vidole – ‘Fingerprint scanner ‘.
Kupitia hii basi hautaitaji kuingiza nywila
(password) kwa kuandika, utaweza fungua
simu yako mara moja baada ya kugususha
kidole husika kwenye scanner hiyo.
Muonekano wa nyuma wa Simu ya Tecno
Phantom 5. Chini ya kamera ni eneo lenye
scanner ya kusoma alama za vidole
Kwa majaribio niliyoyafanya fingerprint sensor
ya Tecno Phantom 5 inafanya kazi kwa haraka
sana – hautasubiri.
Pembeni inamaeneo ya kuzima na kuwasha,
pa kuongezea sauti na pia sehemu ya
kuchomeka memori kadi na pia sehemu ya
kuweka laini za simu (mbili).
Kamera yake na Upigaji picha!
Phantom 5 inakuja na kamera yenye kiwango
cha juu katika eneo la Megapixels, hii ikiwa ni
Megapixel 13 kwa kamera ya nyuma na
megapixel 8 kwa kamera ya selfi na hizi zote
zikiwa na uwezo wa kutoa mwanga wa ziada
(flash).
Ona ubora wa picha zake hapa; (Picha hizi
zilipigwa mida ya asubuhi, jijini Dar es salaam)
Tecno Phantom 5: Kiundani
Tazama video ya uchambuzi wa Tecno
Phantom 5 kutoka kwenye akaunti yetu ya
YouTube.
Laini mbili: Kuna wengi ambao bado wanaona
umefikia muda wa Tecno kutoa matoleo ya
laini moja pia kwa baadhi ya simu zao za
hadhi ya juu kama matoleo ya Phantom.
Phantom 5 inakuja na uwezo wa laini mbili,
(Micro).
Inatumia Programu endeshaji ya Android, toleo
la 5.1 Lollipop… na uchunguzi wa haraka
haraka unaonesha kuna uwezekano watumiaji
wake wakapata sasisho (update) ya
kuwapeleka Android 6.0 – tutachunguza zaidi
kuhusu hili, kama ni la kweli basi ni habari
njema.
Inakuja na diski uhifadhi wa GB 32, ila
utakutana na nafasi ya takribani GB 25 za
kutumia. Nafasi ya kutumia memori kadi
(Micro SD) kunakupa uwezo wa kuweka kadi
ya hadi kufikia GB 128
Inakuja na kiwango cha RAM cha kutosha, hii
ikiwa ni cha GB 3 na hii itasaidia kuhakikisha
hakuna apps zinazokuwa nzito pale
unapoitumia.
Sifa zingine;
Inakubali hadi teknolojia ya 4G LTE
(EDGE, 3G, 4G)
Display – Inchi 5.5 , Pixels 1080 x 1920
(401 PPI), HD, Gorilla Glass 3
Aina ya prosesa: 64 Bit Octa-core 1.3
GHz CPU (Mediatek MT6753)
Prosesa ya Graphics – Mali-T720 (Hii
itasaidia kufanya ubora wa vitu kama
uchezaji magemu uwe mzuri)
Betri la kutochomoa; mAh 3,000
Pia teknolojia zingine zote muhimu
zinapatikana kama vile Bluetooth,
Hotspot (Tethering), WiFi n.k
Mtazamo wa Teknokona
– Kizuri
i. Tecno Phantom 5 ni toleo jingine
linaloonesha ni kwa namna gani kampuni ya
Tecno inaonesha uwezo wake katika
kutengeneza simu za kisasa na zilizobora.
Uwepo wa teknolojia za kisasa kama
Fingerprint Sensor pamoja na utumiaji wa
‘housing’ ya mali ghafi (material) ya bati na
kuachana na maplastiki ni vitu vinavyoipa
Phantom 5 pointi muhimu za ubora. Phantom
5 inamuonekano mzuri.
– Maoni…..
i. Tunadhani muda umefika kwa Tecno katika
baadhi ya simu za hadhi ya juu kama hii kuwe
na matoleo ya laini moja pia. Kuna watumiaji
ambao huwa hawataki kabisa kununua simu
inayotumia laini mbili, kwa sababu zao
wenyewe. Ni vizuri kama mnunuaji akiwa
anataka toleo la Phantom 5 akutane na
chaguo la laini moja au mbili, hili
linawezekana.
ii. Kingine kinachoweza kuwa tatizo kidogo ni
bei yake, kwa wengi bado bei yake inaweza
ikawa ni juu sana ingawa simu inakuja na
ubora wa kuvutia na unaolingana na bei kwa
kiasi flani… Kizuri gharama!
Kutegemeana na ulipo na wauzaji husika, bei
ya Tecno Phantom 5 inacheza kati ya Tsh
700,000 hadi 800,000 | Kes 39,000 – 40,000.
Je ushaitumia au kuiona na kuijaribu simu
hii? Tuambie ni kipi unaona kinafaa
kuboreshwa katika matoleo yajayo ya simu za
Tecno Phantom.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post