TCRA Yaifungia Video mpya ya Wimbo ‘Zigo remix’ ya AY Aliyomshirikisha Diamond Platnumz... SOMA HAPA

Ambwene Yessaya ‘AY’ amethibitisha
kupokea taarifa ya kufungiwa kwa video ya
wimbo ‘ Zigo remix’ aliyomshirikisha
Diamond Platnumz.
Akizungumza na 225 katika kipindi cha XXL
cha Clouds FM, Jumatatu hii, AY amesema
alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa
rafiki yake ambae anafanya kazi katika
chombo kimoja cha habari.
“Sijaelewa maadili gani kwa sababu kama
maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye
swimming pool, na kama kwenye swimmig
pool watu nimevalisha jeans au maturubai
hapo nitakuwa nimekosa maadili,” alisema
AY.
“Mavazi ya kwenye swimming pool yako kila
mahali, hata kwenye taarifa za habari
(Michezo) wanaonyesha waogeleaji, kama hiyo
pia ni kukiuka maadili ni sawa. Inashangaza
mamlaka zetu wanafocus kwenye kufungia
nyimbo zetu na kuacha video za nje. Sijawahi
sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani
umefungiwa, kama wanaona nyimbo za Nicki
Minaj zina maadili halafu Zigo ya AY haina
maadili baasi unaacha tu iwe hivyo ,”
aliongeza AY.
Pia AY alisema barua hiyo ilitoka kwa
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ikisema
kwamba video hiyo inakiuka maadili.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa
TCRA, Innocent Mungi, amethibitisha
kuvitumia vituo vya luninga nchini taarifa ya
namna ya kupembua kazi za wasanii zisizo
na maadili.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post