Hivi karibuni ilivuja sauti ya Dogo Janja akiongea
kwa simu na girlfriend wake ambapo alisikika
akiukashifu uongozi wa TIP TOP kuwa umekuwa
ukiua vipaji vya wasanii wa TI TOP akiwemo
yeye.
Kwa mujibu wa maelezo ya Dogo Janja anadai
sauti hiyo ilirekodiwa bila yeye kufahamu akiwa
anajaribu kumuingiza katika nyavu zake girlfriend
wake, baada ya msichana huyo kumuuliza Dogo
Janja sababu za kupotea katika ramani ya
muziki.
Kwa upande wa Madee ambaye ni msimamizi wa
msanii huyo, ametoa kauli ya utata kuwa
anazielewa hisia za Dogo Janja, wakati huo huo,
ikionekana kuwa wapo pamoja wanafanya kazi
mpya ingawa anakana kukutana na kuzungumza
na msanii huyo kuyaweka mambo sawa baada ya
hitilafu hizo kujitokeza.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon