Tanzania na nchi za Afrika zatakiwa kutilia mkazo uhifadhi wa misitu na wanyamapori.

Mwasisi wa kimataifa wa uhifadhi, Dk Jane
Goodall ameishauri serikali ya Tanzania
kuendeleza juhudi za uhifadhi wa wanyamapori
wakiwemo Sokwe na misitu ambayo ni muhimu
katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi ambazo zimeanza kuathiri ukuaji wa
uchumi na maendeleo ya nchi mbalimbali
duniani.
Akiongea mjini Kigoma kwenye kongamano la
kimataifa la uhifadhi wa mazingira lililoandaliwa
na taasisi yake ya kimataifa ya uhifadhi iitwayo
Jane Goodall Institute, Dk Gane goodall ambae
pia mtafiti wa Sokwe barani Afrika aliyeanza
utafiti huo mwaka 1960 wakati huo akiwa na umri
mdogo, amesema uhifadhi wa misitu ni muhimu
kwani ni sehemu ya makazi ya wanyamapori na
viumbe adimu wakiwemo Sokwe ambao
wanafanana kijenetiki na mwanadamu kwa zaidi
ya asilimia 98 na ameikumbusha serikali ya
Tanzania kuendelea kuheshimu maeneo
yaliyohifadhiwa kwani yana rasilimali muhimu
ikiwemo vyanzo vya maji.
Nae mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya uhifadhi ya
Jane Goodall upande wa Tanzania James
Lembeli amesema anayo imani na rais Dk John
Pombe Magufuli katika masuala ya uhifadhi na
amezungumzia umuhimu wa maeneo ya Gombe
na Mahale ambayo ni makazi pekee ya Sokwe
kwa Tanzania na ameishauri serikali kukubali
kuyaingiza maeneo hayo katika hadhi ya maeneo
ya uridhi wa dunia ili yaweze kupewa kipaumbele
na kutambuliwa na taasisi za kimataifa za
uhifadhi.
Wakiongea kwenye kongamano hilo, wakuu wa
mikoa ya Kigoma na Katavi, kanali mstaafu Issa
Machibya na Dk Ibrahim Msengi ambao pia
wameshiriki kwenye uzinduzi wa mpango wa
kielekroniki wa ufutiliaji wa masuala ya uhifadhi
na uharibifu wa mazingira kwa njia ya setelite
wamepongeza mchango mkubwa wa taasisi ya
Jane Goodall katika uhifadhi wa mazingira nchini
na kwamba zoezi la kuwaondoa watu wanaoishi
kwenye maeneo yaliyohifadhiwa likiendelea
litasaidia kuimarisha uhifadhi katika mikoa hiyo
ya Kigoma na Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post