Moto wateketeza mashamba ya Miwa Zanzibar

Hekari zaidi ya 100 za mashamba ya Miwa
zimeteketea kwa moto katika kile ambacho
wamiliki wa mashamba hayo wamedai ni njama
za makusdi zinazofanywa na watu au kikundi
maalum.
Tukio hilo la kuteketeza kwa mashamba hayo ya
Miwa ambayo yako katika kiwanda cha sukari
kiliko Mahonda mkoa wa kaskazini Unguja
ambacho kinaendeshwa na wawekzaji kutoka
India ambapo hili ni tukio la tano kutokozea
katika kipndi cha miezi miwili na kusababisha
hasara ya mamilioni ya fedha.
Akizungumza na vyombo vya habari afisa
utumishi wa kiwanda hicho ambacho kinara kwa
kuzalisha sukari hapa Zanzibar Bashiir Mohmaed
amesema moto huo ni njama zinazofanywa na
watu au kikundi kwa maksudi huku wao
wakishindwa kujua sababu za mashamba hayo
ambayo yalikuwa tayari kwa kuvuna Miwa na
kuanza uzalishaji.
Mkuu huyo wa utumishi amesema kiwanda hicho
ambacho kinatoa ajira kwa zaidi ya watu 300
kinalazimika kufungwa kutokana na hali hiyo
amabyo amesema ni hasara kwa wawekazaji na
wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo mmoja ya mlinzi wa kiwnada hicho
mzee Saidi Mussa ambaye yuko kwa miaka mingi
kiwandani hapo amesema iko haja ya pande
zote kukaa pamoja na kutafakari nini tatizo la
mara kwa mara kuwepo kwa moto.
Katika ajali hiyo ya moto ya mwisho ilishuhudiwa
na viongozi wa seriklai akiwemo mkuu wa mkoa
wa kaskazini ambaye alikuwepo kuangalia tatizo
hilo huku kamnada wa polisi wa mkoa wa
kaskazini Mohmaed Msangi katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari amesema polisi
wanawashikilia watu wawili na uchunguzi bado
unaendelea.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post