Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wamehimizwa
kulima mazao yanayohimili ukame yakiwemo
Mihogo, Mtama na Viazi lishe ili kukabiliana na
janga la njaa linalosababishwa na mabadiliko ya
tabianchi hali inayotokana na kukatwa miti ovyo
na uharibifu wa mazingira.
Hayo yamesemwa na mjumbe wa halmashauri
kuu ya CCM kutoka wilayani Kishapu
Bw.Boniface Butondo katika kilele cha
maadhimishi ya sherehe ya kuzaliwa chama cha
mapinduzi maadhimisho yaliyofanyika kimkoa
katika kata ya Oldi Shinyanga.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw.Ally
Nasoro Rufunga amewataka watumishi wa
serikali kuanzia ngazi za vijiji hadi mkoa kutenda
kazi kwa bidii na uwajibikaji zaidi ili kutimiza
lengo la serikali ya awamu ya tano huku
akisisitiza wanafunzi waliofaulu kuingia kidato
cha kwanza mwaka huu waende shuleni na
kutangaza hali ya hatari kwa mtu yeyote
atakayeoa mwanafunzi na kuwataka wazazi
kuhakikisha wanasimamia jambo hilo sawasawa
kama serikali ilivyotoa maagizo.
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kaimu
katibu mkuu wa CCM Kahama Bi. Alexadrina
Katabi amewataka watanzania bila kujali itikadi
za vyama, dini na hata ukabila kufanya kazi kwa
kushirikiana huku akikumbushia kaulimbiu ya
serikali kwamba hapa kazi tu! Ambapo hafla hiyo
ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo mbio
za basikeli na mchezo wa mpira wa miguu.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon