Makamu wa rais, Mh Samia Suluhu Hassan,
ameyataka mashirika mbalimbali nchini hasa
sekta binafsi kuwaingiza wanawake kwenye bodi
ili kukuza uchumi, kuongeza kipato cha wananchi
na kuondokana na umasikini.
Mh Samia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akifungua mpango wa kutoa mafunzo
ya uongozi kwa wanawake, namna ya kufanya
kazi, kuongoza nafasi za ukurugenzi na bodi
mbalimbali, ulioandaliwa na chama cha waajiri
Tanzania ATE.
Waziri wa sera, bunge, kazi, vijana, ajira na
walemavu Mh Jenista Mhagama akizungumza
katika uzinduzi huo amesema asilimia kubwa ya
nguvu kazi iko sekta isiyo rasmi hivyo ameitaka
ATE kufikiria namna ya kugawa huo mpango
kusaidia wanawake ngazi ya chini.
Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa ATE
Dk Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa ATE Afrika
Almas Maige amesema mpango huo utawezesha
wanawake kupata mafunzo ya namna ya
kusaidia kuwa wakurugenzi wa bodi na kuingia
kwenye nafasi za kufanya maamuzi makubwa na
yataanza kutolewa kwa walimu.
Uncategories
Makamu wa rais Mh.Samia Suluhu azindua
mpango wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa
wanawake DSM.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon