Serikali yavunja mkataba wa kiwanda cha Mponde

Awali akitangaza kuvunjwa kwa mkataba huo
rasmi msajili wa hazina kutoka ofisi ya msajili wa
hazina Laurence Mafuru amesema wamevunja
rasmi mkataba huo kutokana na kukiukwa kwa
makubaliano waliyowekeana na mwekezaji huyo
kushindwa kuyatekeleza ipasavyo.
Aidha amesema kwa muda wa miaka mitatu sasa
kiwanda hicho kilisimama kufanya shughuli za
uzalishaji kutokana na mgogoro uliokuwepo baina
ya wakulima na mwekezaji huyo hali iliyopelekea
wakulima wa zao hilo kuyumba kimaisha.
Mafuru amesema lengo la serikali ni kuhakikisha
inafufua na kuviendeleza viwanda vilivyopo
Nchini kwa maslahi ya wananchi wake ikiwa ni
pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja
sambamba na kuinua uchumi wa eneo husika.
Amesema serikali ilifuata taratibu na sheria ya
kusitisha mkataba huo hivyo wametengeneza
menejimenti ya muda mfupi itakayoendesha na
kuboresha kiwanda hicho chini ya usimamizi wa
bodi ya chai ili kianze kazi ya uchakataji chai
kwa haraka.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post