Wakazi wa jiji la Mbeya leo wamejikuta katika
wakati mgumu kwa kukosa usafiri wa kuingia na
kutoka katikati ya jiji baada ya madereva wa
daladala zinazofanya safari zake kati ya Uyole na
Stendi kuu kufanya mgomo ambao umeambatana
na vurugu kubwa wakipinga njia wanazopita kwa
madai kuwa ni mbovu, hali ambayo imesababisha
jeshi la polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa
mabomu ya machozi.
Madereva wa daladala zinazofanya safari zake
kati ya Uyole, Isyesye na Ituha uelekea maeneo
ya Majengo na Stendi kuu jijini Mbeya leo
wamefanya mgomo ambao umeambatana na
vurugu kubwa wakipinga kupita kwenye barabara
kadhaa ambazo wamepangiwa na Sumatra kwa
madai kuwa barabara hizo ni mbovu na hazina
vituo vya kupakia na kushusha abiria.
Kutokana na vurugu hizo jeshi la polisi limeamua
kuingilia kati kwa kuwatawanya madereva hao
kwa mabomu ya machozi na akizungumzia
mgomo huo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,
kamishna msadizi mwandamizi wa jeshi la polisi,
Ahamed Msangi amewataka wakazi wa jiji la
Mbeya kuwa watulivu akisema kuwa hakuna
sababu za kufanya fujo kwa sababu malalamiko
ya madereva hao ni jambo linazozingumzika huku
akidai kuwa anaamini kikao cha dharura
ambacho kimeitishwa na mkuu wa mkoa wa
Mbeya Abaas Kandoro kikihusisha wadau wote
wa usafirishaji kitatoa ufumbuzi wa tatizo hilo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon