Mke wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Janeth Magufuli ametemelea
kituo cha makazi ya wazee na walemavu
wasiojiweza Nunge Kigamboni jijini Dar es
Salaam, na kushuhudia wazee hao na walemavu
wakiishi maisha magumu kutokana na huduma
duni ikiwemo ukosefu wa chakula cha uhakika.
Akiwa na mwenyeji wake mkuu wa wilaya ya
Temeke Bi Sophia Mjema, Mama Janeth Magufuli
baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ya
makazi ya wazee hao, alipata fursa ya
kuzungumza nao ambapo ameiomba jamii kwa
ujumla kujenga tabia ya kuwasaidia watu
wasiojiweza kwani kwa kufanya hivyo ni njia
moja wapo ya kutimiza agizo la mungu ambalo
linasema ukimsaidia maskini unamkopesha
mungu.
Kutokana na uvamizi wa baadhi ya maeneo ya
makazi ya wazee na walemavu hao, Mama
Janeth amemuomba mkuu wa wilaya ya Temeke
kuakikisha kuwa wanashughulikia tatizo hilo ili
waliovamia maeneo hayo wachukuliwe hatua za
kisheria ikiwemo kuondolewa katika makazi hayo.
Wazee hao wakiongozwa na mwenyekiti wao
mzee Anthony Francis Kikongoti, mbali na kutoa
shukrani zao kwa Mama Janeth Magufuli kwa
kuwaletea Unga kilo 3000, Mchele kilo 3000 na
Maharage kilo 1200 ambapo kila mtu atapewa
kilo 25 ya mchele na unga kilo 25 pamoja na kilo
10 ya Maharage ili kuwasidia,wameeleza ukweli
kwamba wamekuwa wakiishi maisha ya tabu na
kwamba serikali ya awamu ya tano imeanza
vizuri kwa kuwajali wanyonge ili wajisikie furaha
katika nchi yao.
Uncategories
Mke wa rais Mama Janeth Magufuli
ametemelea kituo cha wazee na walemavu
wasiojiweza Nunge Kigamboni DSM.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon