Serikali ya Tanzania kuwezesha wananchi kiuchumi

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza
Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la
kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na washiriki wa Mkutano wa
Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi nchini uliofanyika , jijini Dar es Salaam.
Mhe. Majaliwa amesema maeneo yanayolengwa
na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya
haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa
katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu,
ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na
usafirishaji.
Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025
inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya
uchumi wa nchi inamilikiwa na Watanzania
wenyewe.
Katika Mkutano huo Waziri Mkuu pia alizindua
Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post