Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi CCM
imefanya uteuzi mpya wa nafasi za uenyekiti
zilizoachwa wazi kati ngazi ya mikoa na wilaya
ambapo viongozi hao walijiunga na Vyama vya
Upinzania pamoja na wengine kufariki dunia.
Akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar
es Salaam katibu wa itikadi na uenezi wa chama
hicho Mhe. Nape Nnauye amesema uteuzi huo
umetokana na vifo pamoja na baadhi ya viongozi
kuhamia vyama vya upinzani wengi wao
wakihamia Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA).
Nape amesema mikoa mitatu wenyeviti wake
walihama imeshapata wagombea wa nafasi hizo
ambapo ni mkoa wa Shinyanga alipokuwepo
mwenyekiti Khamis Mgeja, Arusha, Onesmo Ole
Nangole, na Mgana Msindai wa Singida ambao
wote walihamia UKAWA.
Mhe. Nape aliwataja wagombea wa nafasi hizo
zilizoachwa wazi kuwa ni Michael Lekule,
Emanuel Lusenga na John Pallangyo uenyekiti
Arusha, Mkoa wa Shinyanga ni Hassan
Mwendapole, Mbala Mlolwa na Eraso Kwilasa
(Uenyekiti), Mkoa wa Singida, Hanje Barnabas,
Misanga Hamis, Martha Mlata na Kilimba Juma
(Uenyekiti).
Aidha Nape amesema nafasi nyingine zilizojazwa
ni pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha Mkoa
wa Kilimanjaro, Katibu wa siasa na uenezi Mkoa
wa Arusha na uenyekiti wa vijana CCM, mkoa
nazo zitazibwa,
Mbali na hizo nafasi nyingine ambazo zitazibwa
baada ya kuachwa wazi kutokana na sababu
mbalimbali ikiwamo ya viongozi kuihama CCM na
vifo ni zile za ujumbe wa Halmshauri Kuu ya
CCM, Taifa na uenyekiti wa CCM wilaya.
EmoticonEmoticon