Serikali imeamua kuanzisha kikosi maalum cha kukabiliana na ujangili nchini.

Waziri wa mali asili na utalii Mh Profesa
Jumanne Maghembe amesema kutokana na tukio
lilotokea la kushambuliwa kwa helkopta ya doria
na kuuwawa kwa rubani Rogers Gower serikali
imeamua kuanzisha kikosi maalum kwa
kukabilina na ujangili kikosi ambacho kitahusisha
idara zote za wizara hiyo.
Mh. Maghembe ameyasema hayo alikupokutana
na mkuu wa jeshi la polisi nchini na vionozi
mbalimbali kwa lengo la kuzungumzia mikakati
hiyo ya serikali.
Naye mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest
Mangu amesema jeshi lake litaanza operesheni
maalum ya kukamata silaha zote ambazo
zimetolewa kihalali lakini zinatumika kufanya
ujangili.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post