Bunduki hiyo aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na
63229, imepatikana mara baada ya jeshi la polisi
kufanikiwa kuwakamata watu 9 wanaotuhumiwa
kuhusika na tukio hilo.
Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa
kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na
jeshi hilo kushirikiana na wananchi, pamoja na
uongozi wa TANAPA.
Aidha waliokamatwa wamekiri kuhusika na tukio
hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa
ulifanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio
kutokea chini ya mkuu wa upelelezi mkoa
Jonathan Shana.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon