Rais wa Zanzibar Dkt. Shein azindua mahakama ya watoto.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein ameitaka jamii
nchini kupambana na ukatili na udhalilishaji wa
watoto kwa vitendo na sio kukemea pekee.
Dr. Shein ametoa changamoto hiyo huko mkoa
wa kaskazini Unguja wakati akizungumza na
wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi na
kuizindua rasmi kazi ya ujenzi wa jengo la
mahakama maalum ya kusimamia kesi
zinazohusu watoto ambapo amesema vita hivyo
ni vikubwa na jamii lazima iungane pamoja huku
akionekana kushangazwa na watu wenye tabia
hizo za kubaka na kudhalillsha watoto.
Mapema jaji mkuu wa Zanzibar Mhe Othman
Makungu amesema kuwepo kwa jengo hilo
kutapunguza misongamano wa kesi katika
mahakama kuu huku akisema jengo hilo litakuwa
maalum na watoto watakuwa huru bila ya uoga
huku mrajis wa mahakama kuu Mhe George Kazi
amesema jengo hilo linatarajiwa kumalizika
mapema mwezi ujao na shilingi miloni 100
zinatarajiwa kutumika na mipango iko mbiono
kwa pemba kuwa na mahakama kama hiyo.
Kesi za udhalilishaji na ubakaji wa watoto ni
moja ya tatizo sugu kiswani Zanzibar huku
tathmni zikionyesha kesi za jinai zinazohusu
watoto zimefunguliwa kati ya hizo 54 za makosa
ya jinsia na udhalilishaji kijinsia watoto ingawa
pamekuwa na mafanikio ya kuwepo kwa
wananchi kuripoti matukio 1049.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post