Hali ya wananchi Kilosa ni mbaya sana - prof J

Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule
(CHADEMA ) maarufu kama prof J amesema hali
ya wananchi katika jimbo lake hususani wananchi
wa kata ya Tindiga wilayani Kilosa ni mbaya
sana kutokana na mafuriko kusomba nyumba zao
zaidi ya 600.

Haule ameyasema hayo alipokuwa akizungumza
na blog kuhusiana na hali ya wananchi wa jimbo
lake ambao wamekumbwa na mafuriko na
kusababisha zaidi ya kaya 5000 kukosa makazi
na kuhifadiwa na ndugu zao huku wengi
wakihama maeneo na wengi wakikosa pa
kujihifadhi.
''Hali ni mbaya sana maji hayo yanatokana na
mto Mpwapwa kupasuka kingo zake, pamoja na
kupasuka kwa bwawa la Kidete baada ya
kuzidiwa na maji hivyo maji hayo moja kwa moja
yanafika kwenye makazi ya wananchi na kufanya
wawe wahanga na kutafuta namna ya
kujilinda''Amesema Prof. J
Haule ameongeza kuwa wanafunzi wamekwama
kimasomo lakini pia huduma nyingine nazo ni
ngumu kupatikana pia ugonjwa wa kipindupindu
upo hatarini kuongeza kasi mkoani Morogoro kwa
sababu baada ya mafuriko hayo wananchi nao
wametapisha vyoo hivyo kipindupindu ni rahisi
kulipuka.
Aidha mbunge huyo amesema yeye amepeleka
msaada wa awali wa maji ya kunywa lita elfu 13
na anaomba msaada kwa serikali na yeyote
mwenye mapenzi mema kuweza kujitolea
mahema, chakula na dawa kwa ajili ya
kuwasaidia wananchi hao.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post