Halmashauri ya Mji wa Geita kwa
kushirikiana na Polisi wamefanikiwa kumtoa
Mwalimu Hamis Mumwi aliyekuwa akiishi
darasani katika shule ya msingi Mwagimaji.
Mwalimu Mumwi ameishi kwa takribani
miaka 10 darasani na familia yake baada ya
kufukuzwa kazi kwa madai ya kumpa
mimba Mwanafunzi na Kumuoa ambapo
aligoma kutoka katika darasa hadi
Halmashauri imlipe stahiki zake.
Halmashauri imechukua hatua hiyo baada
ya kuona mwalimu huyo hana stahiki
anazodai kwa kuwa alishalipwa na
kupelekwa kwao ukerewe.
Inadaiwa kuwa Halmashauri ilitafuta
msaada kwa Polisi ambapo Mumwi alihojiwa
na kutakiwa kuondoka darasani ambapo
alihamisha vitu vyake katika nyumba
alokuwa anaishi zamani ambayo imebomoka
upande.
Walimu na Diwani wa Kata ya Nyanguku
Elia Ngole wamekishukuru kituo cha
Habari kwa kuwasaidia kutatua tatizo
waliokuwa nalo kwa muda mrefu.
Katibu idara ya utumishi wa walimu TSD
Khalid Shaban amesema Mumwi
hajafanyiwa hujuma kama anavyosema bali
alifukuzwa kulingana na kosa na taratibu
zilifuatwa na alipewa haki ya kujieleza na
shauri lake kwenda mamalaka ya juu na
kufukuzwa kazi.
Akizungumza kwa njia ya simu Mumwi
amesema ameondoka katika darasa hilo na
kudai bado anahaki zake anazifatilia.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon