Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
amemtaka jaji kuu wa Tanzania kutumbua majibu
kwa kuwafukuza kazi mahakimu wote
walioshindwa kufikia masharti yaliyowekwa ya
kutoa hukumu 260 kwa mwaka kwa kuwa
wanachangia kuondoa sifa ya nzuri ya
mahakama.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa
mwaka mpya wa mahakama, Dkt Magufuli
amesema bila ya kuchukua hatua hakuna
kitakachofanyika kwa kuwa mambo
yanayofanyika ndani ya serikali ni ya ajabu na
yanaondoa sifa ya taifa la Tanzania.
Akizungumzia na viongozi wa serikali na taasisi
za serikali wanavyofanya ufisadi wa fedha za
walipa kodi Dkt Magufuli amesema.
Kuhusu udhahifu uliopo kwa upande wa ofisi ya
mkurugenzi wa mashtaka -DPPO- rais Dkt John
Pombe Magufuli amesema haiwezekani
mtuhumiwa anakamatwa na kidhibiti mikononi na
kesi inachukua miaka kwa madai ya uchunguzi
kutokamilika.
Kwa upande wake jaji mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohamed Othumani Chande amesema
mahakama inatarajia kuanza kusikiliza kesi za
uchaguzi wa madiwani na wabunge kuanzia
Februari 22 mwaka huu ambapo mashauri 221 ya
kupinga matokeo ya uchaguzi yasikilizwa na
jumla ya shilingi bilioni 3 zinahitajika, ambapo pia
amesema mahakama iko katika mchakato wa
kuanzisha mahakama maalum ya wahujumu
uchumi na mafisadi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon