Polisi DSM yawakamata watuhumiwa 21, kwa makosa ya ujambazi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es
Salaam imewakamata watuhumiwa 21 kwa
makosa ya Ujambazi wanaotumia silaha.
Musa Said, Mohammed Ally Chinga na
Almas Daudi ambao ni wakaazi wa jiji la Dar
Es Salaam na ni miongoni mwa majambazi
Sugu wanaodaiwa kufanya matukio tofauti
ya uhalifu.
Polisi pia wamesama wamekamatwa na
bunduki mbili aina ya Browning na Berreta
pamoja na Risasi tatu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum
ya Dar Es Salaam Simon Sirro ameonyesha
Leseni za Biashara ambazo hazijatajwa
majina ya wamiliki, Plate namba za Pikipiki
sita tofauti na Vivuli vya kadi za magari na
pikipiki.
Kupitia Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na
wezi wa Magari cha Polisi Kanda Maalumu
ya Dar Es Salaam limewakamata
watuhumiwa wawili kwa makosa ya
kughushi Nyaraka bandia za Umiliki wa
Magari na Leseni.
Kamanda Sirro amewataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza
kuwabaini wahalifu mapema ,ili kupunguza
matukio ya uhalifu nchini.
Katika hatua nyingine Jeshi kanda Maalumu
ya Dar Es Salaam inawatafuta watuhumiwa
wanne kwa makosa ya wizi katika mashine
za kutolea fedha, ambo wanaongozwa na
raia wa Congo,ambao wamekuwa wakifanya
uhalifu huo katika benki mbalimbali nchini.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post