Watu watatu wamedungwa visu katika mapigano
kati ya kundi linalowachukia watu weusi la Ku
Klux Klan (KKK) na waandamanaji
wanaowapinga katika jimbo la California.
Tukio hilo lilitokea karibu na eneo kulikopangwa
mkutano wa hadhara wa wazungu wao
wanachama wa KKK.
Watu wanne walitiwa mbaroni katika makabiliano
hayo, akiwemo mwanachama mmoja wa KKK
aliyemdunga mweusi kisu.
Msemaji wa polisi alieleza kuwa shida ilianza
wakati wanachama wa KKK waliwasili katika
uwanja wa Anaheim, karibu kilomita 50 Kusini
Mashariki mwa Los Angeles, karibu na
Disneyland.
Msemaji wa polisi alisema kuwa wanachama hao
wa KKK walishambuliwa weusi walipokuwa
wanatoka kwenye gari.
Mmoja aliangushwa chini.
Waandamanaji watatu wanaopinga KKK
walidungwa visu katika makabiliano hayo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia matukio hayo alisema
kuwa wanachama wa KKK walikuwa
wamelemewa.
Mmoja wa waliodungwa visu anaugua na
amelazwa hospitalini.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon