Msanii machachari anayefanya poa kwenye
runinga za bongo kupitia filamu Elizabeth Michael
au Lulu, amemuwakia mtu aliyepost kuwa
amefariki na kuwataka watu wakaone picha za
msiba wake, na kusema hafi mpaka siku za
kwenye biblia ziishe.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Lulu
ameandika maneno hayo huku akionyeshwa
kuchukizwa na kitendo hicho cha kuzushiwa kifo,
na kujisifia kuwa ana jina maarufu.
"Nasikia Nimekufa, wewe uliye Post hii Kama
wewe utakuwepo tutaonana tena 2017
Inshaallah, halafu jifunze na kuandika Elizabeth
vizuri kwanza (Niki report live kutoka heaven),
this shows how jina langu lina KiKi, nishasema
mniache jamani, kufa ntakufa sikatai lakini
mpaka nimalize miaka iliyoandikwa kwenye
biblia", aliandika Lulu.
Maneno hayo ya Lulu yameibua hisia za watu na
kumjia juu mtu aliyepost taarifa hiyo kwenye
mitandao, huku wakimtaka Lulu kutopigizana nao
kelele kwani yeye ni kioo cha jamii hivyo ni
kawaida kwa kuzushiwa taarifa za uongo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon