Ajali ya basi mkoani Mara.

Watu saba wamafariki wamefariki dunia na
wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya baada ya
basi la abiria la nata raha yenye namba za usajili
T 473 CJN linalofanya safari zake kati ya
Mugumu wilayani serengeti kupitia Bunda
kwenda mkoani Mara kupalamia nyumba eneo
la njia nne mjini Bunda baada ya breki za basi
hilo kukatika likiwa katika mteremko mkali.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe, ambaye
pia ni mkuu wa wilaya ya Bunda, akizungumza
baada ya kufika eneo la tukio, amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa tano asbuhi
na kusema kati ya majeruhi hao wanane
wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini
Mwanza huku wengine wakilazwa hospitali teule
ya DDH mjini Bunda.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamedai baada
ya kukaribia njia kuu ya Mwanza Musoma mita
chache tu kufika kituo kikuu cha mabasi
mjiniBunda mwendo wa basi hilo uliongezeka na
baada ya kuhoji walielezwa kuhusu kukatika kwa
breki hizo kabla ya kuvamia jengo hilo.
Hata hivyo wakati mwenyekiti huyo wa kamati ya
ulinzi na usalama akisema walifariki ni abiria
saba lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mara
ACP Philip Alex Kalangi
kwa njia ya simu amesema abiria sita ndiyo
waliofariki katika ajali hiyo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post