Ray C amesema hayo kupitia kipindi cha eNews
na kusema toka ameachana na msanii Lord Eyes
hajawahi kuingia tena kwenye mahusiano na
kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana mpaka
yeye kuingia kwenye matumizi ya dawa za
kulevya kipindi hicho.
"Kwa sasa bado sina boy friend, now nina
marafiki tu kiukweli nafasi hiyo bado maana Lord
Eyes aliniumiza sana, nilimpenda sana na ndiyo
maana nilifanya alichokuwa akifanya,
sikutegemea kama ingekuwa vile, hata kwenye
drugs unakutana na rafiki yako anafanya hiki na
wewe utataka kufanya ili aone upo naye pamoja,
ila kwa sasa mimi na wasanii hapana, ni bora
hata nitoke na msukuma mkokoteni ili mradi
anipende maana mimi nina mapenzi ya kweli
ndiyo maana unaona hata nyimbo zangu nyingi ni
za mapenzi" Alisema Ray C.
Ray C amekuwa akijutia sana suala la mapenzi
na kukiri wazi kuwa hilo ndiyo jambo
lililompelekea kuingia kwenye matumizi ya dawa
za kulevya kwa kipindi cha nyuma kabla ya
kuanzishiwa dozi kwa ajili ya kuachana na dawa
hizo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon