Hali ya usalama katika eneo la Kigogo
Mkwajuni jijini Dar es Salaam ni tete kutokana na
wananchi wa eneo hilo kuvamiwa nyakati za
usiku na kundi la vijana kwenye silaa za jadi na
kuwaibia mali zao ambapo ITV imefanikiwa
kuonana na familia mbili ikiwemo ya Bwana
Erinest Mahiga ambaye amekatwa na mapanga
wakati akijaribu kukabiliana na wezi hao baada
ya kumvamia usiku.
Familia ya pili ni ya Bwana Ananias Felix ambayo
imeibiwa fedha pamoja na samani mbalimbali za
ndani.
ITV inaendelea kufanya juhudi kuongea na diwani
wa eneo hilo pamoja na mwenyekiti wa serikali
za mtaa ili kufahamu mstakabali wa wananchi
katika kuimarishiwa ulinzi ikiwemo swala la ulinzi
shirikishi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon