Mwigulu awasili eneo la mapigano yaliyoua mbuzi 75

Mapigano ya wakulima na wafugaji Morogoro
kata ya Hembeti ,Kijiji cha Kigurukwa,Kitongoji
cha Dihamba chasababisha mauaji ya mbuzi 75
waliokatwakatwa kwa mapanga, Waziri wa
Kilimo,Uvuvi na Mifugo bila kuchelewa awasili
eneo la tukio na kuchukua hatua Mh. Mwigulu Nchemba ameagiza kamati ya
Ulinzi ya mkoa na wilaya kuhakikisha waliofanya
uharibifu huo wakamatwe haraka sana.
Pili ameagiza kupitia hukumu ya mahakama
iliyotolewa mwaka 2015 kuweka mipaka kati ya
eneo la wakulima na wafugaji itekelezwe haraka
iwezekanavyo.
Mwisho Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza
kuwepo mkutano wa hadhara wa wakulima na
wafugaji na viongozi wote wa serikali wa wilaya
na mkoa tarehe 20/02/2016 ndani ya kata ya
Hembeti.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post