Mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea
urais wa Zanzibar, Mohamed Sultan
Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami,
amewekwa ndani na Jeshi la Polisi mjini
Unguja kwa tuhuma za kumtukana Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Eddy Riyami ambaye ni mmoja wa wana
mkakati wa timu ya ushindi wa aliyekuwa
mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad, alikutwa na mkasa huo jana baada
ya kuitwa polisi kutoa maelezo kutokana na
tuhuma zinazomkabili.
Riyami ambaye pia alikuwa Mjumbe wa
Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alikwenda
Polisi Makao Makuu kuitikia wito wa Naibu
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua, huku
akiandamana na Mwanasheria wa CUF,
Masoud Faki Masoud.
Mwanasheria huyo jana alisema Riyami
anatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya
ya kimtandao.
Alisema licha ya kuzikana tuhuma hizo,
lakini Jeshi la Polisi bado lilimshikilia kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
“Ni kweli ameshikiliwa na polisi kwa ajili ya
kupitisha uchunguzi na yupo Polisi Madema,
eti Eddy kaambiwa kamtukana Dr. Shein
kwenye ‘audio’ ambayo hata si sauti yake,
lakini dhamana ipo wazi na tutamchukulia
dhamana,” alisema Masoud.
Akizungumzia kukamatwa kwa Riyami, Naibu
Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya
Jinai, Salum Msangi, alithibitisha kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
“Kitu ninachoweza kuthibitisha ni kuwa
tunamshikilia Riyami kwa ajili ya kupitisha
uchunguzi,” alisema Naibu Kamishna
Msangi.
Februari 15, mwaka huu Ofisi ya Mkurunzi
na Makosa ya Jinai, ilimwandikia Riyami
barua ya wito na kumtaka kufika ofisi ya
upelelezi iliyopo Makao Makuu ya Polisi
Zanzibar.
Riyami alitii wito huo ambapo wiki iliyopita
alikwenda lakini mmoja wa maofisa wa
Jeshi la Polisi aliyemwandikia barua alikuwa
nje ya Zanzibar kwa shughuli za kikazi na
kumtaka kwenda jana jumatatu
Riyami si mwanachama wa CUF, lakini mara
kadhaa amekuwa akitumiwa na chama hicho
kwa ajili ya mikakati mbalimbali pamoja na
ushauri.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon