Mengi yazidi Kuibuka Kuhusu Nyalandu na Kampuni ya Uwindaji Ambayo Majangili Walitungua Helkopta yao na Kuuwa Mzungu

Mambo mapya yameibuka kuhusu kampuni
ya Kimarekani ya Friedkin Conservation
Fund (FCF) ambayo majangili walidungua
helikopta yake mwezi uliopita na
kusababisha kifo cha rubani raia wa
Uingereza, Roger Gower.
FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa
kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania
Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd na
Wengert Windrose Safaris.
Wakati helikopta hiyo ikidunguliwa kwa kile
kinachoelezwa kwamba ilikuwa kwenye doria
dhidi ya majangili, kumbukumbu zilizopo
Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonesha
kuwa kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni
miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio
kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba
kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori
na kukutwa na nyara za Serikali.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara
ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote
kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama
kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni
urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri
wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.
Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni
hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia
moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio
za kuwania urais, kabla ya kushindwa na
kujielekeza kwenye ubunge. Helikopta
iliyodunguliwa na majangili ndiyo aliyoitumia
wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul
Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia
ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi)
kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu
vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni
hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa
kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio
katika hatari ya kutoweka.
Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza
ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa
kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu
vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo
ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria
ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu
kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu
kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza
na waombaji washindanishwe katika mfumo
na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni
ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).
Pamoja na kutoa Leseni ya Rais,
Wamarekani hao walileta watoto wadogo,
chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo
ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3)
cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya
mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha
shughuli za utalii kwenye eneo la Makao
WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings
Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya
Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na
wanyama (Makao Ranch).
Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya
TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin
Conservation Fund (FCF) imekuwa
ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la
Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba
Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na
WMA ya Makoa kwa ajili ya shamba la
mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na
JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings
Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo
la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha
sheria.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post