Mramba na Yona waanza kutumikia kifungo cha kufanya usafi hospitali Sinza Palestina.

Aliyekuwa waziri wa fedha, Basil Mramba na
waziri wa nishati na madini, Daniel Yona,
mapema leo wamewasili katika hosptali ya
Palestina Sinza jijini Dar es Salaam kuanza
kutumikia kifungo chao cha nje kwa kufanya
usafi katika maeneo ya kijamii.
Mawaziri hao wa zamani walikuwa wanatumikia
kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la
matumizi mabaya ya ofisi na kuisababisha
serikali hasara walibadilishiwa adhabu ya jela na
kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha nje
mwishoni mwa wiki iliyopita na mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu, baada ya kukamilika
mchakato wa kufikia hatu hiyo.
Baada ya kuwasili hospitalini hapo, Yona na
Mramba walipokelewa na ofisa huduma za jamii
Bw. Deogratius Shirima na wananchi wengine
waliokuwepo kushuhudia vigogo hao wakitumikia
adhabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini
hapo, Shirima alisema kuwa, leo ilikuwa ni siku
ya kuwapa maelekezo namna ambavyo
watafanya usafi, maeneo ya kufanya usafi pia
walikabidhiwa vifaa watakavyovitumia kufanyia
usafi kuanzia kesho.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post