Kamati ya maafa nchini yatakiwa kuongeza misaada mkoani Tabora.

Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora
imetoa rai kwa kamati ya maafa nchini kuongeza
misaada mbalimbali ili kuwawezesha wananchi
wahanga wa mvua wilayani humo wanaoendelea
kukumbwa na changamoto ya nyumba zao
kubomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha
mkoani Tabora.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Bw, Said Shabani Ntahondi
wakati akikabidhi maturubai zaidi ya mianne ili
kuwawezesha wahanga wanaoendelea kulala nje,
ili wapate sehemu ya kujikimu, kwa kuwaondolea
adha ya kunyeshewa mvua.
Aidha afiasa kilimo wilayani humo Bw, Absalom
Kajuna amesema kuwa, poamoja na juhudi za
halmashauri kupeleka misaada ya awali bado
kuna changamoto kubwa ya kuwafikia wahanga
kutokana na miundombinu kuharibika sana
ambapo zaidi ya kata kumi zinaendelea
kuathiriwa na mvua.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post