Miili ya askari 3 waliokufa katika msafara wa rais yaagwa mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida ameongoza maelfu ya
wakazi wa mkoa wa Singida pamoja na askari
wa jeshi la polisi kwenye kuaga miili mitatu ya
maafisa wa jeshi la polisi waliokufa kwenye
ajali wakati wakisindikiza msafara wa rais.
Akitoa salamu kwa niaba ya rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mheshiwa Dkt John
Pombe Magufuli, mkuu wa mkoa wa Singida
dakari Parseko Kone amesema rais amepokea
msiba huo kwa masikitiko makubwa na
amewatakia familia za marehemu kuwa na moyo
wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Akieleza ajali ilivyo tokea kamanda wa polisi
mkoa wa Singida ACP Thobiasi Sedoyeka
amesema gari lilikuwa likiongoza msafara wa rais
lilipasuka gurudumu lambele upande wa kulia na
dereva sajent Gerald Ntondo kushindwa kuli
mudu, huku akitoa salamu kwa niaba ya
makamda wa polisi Tanzania, kamnda wa polisi
mkoa wa Manayara ACP Kamilius Wambura.
Kwa upande wao viongozi wa madhehebu ya dini
ya kikristo na kiislamu wamewata waumini
kujiandaa mapema kwa sababu hawajui siku wa
saa ambayo bwana atawa kuja chukuwa.
Akitoa wasifu wa marehemu hao mnadhimu mkuu
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Simon
Haule amesema jeshi la polisi mkoani Singida
limepoteza askari ambao walikuwa wana
tegemewa katika utendaji wao wa kazi na miili
hiyo ina safirishwa kwenda kwa maziko Miraji
Mwegoro mkoa wa Dar-es-Salaam, Eliasi Mrope
mkoa wa Mtwara na Geradi Ntondo mkoa wa
Kigoma.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post