Serikali yakipongeza kiwanda cha Bonite kwa uzalishaji wa bidhaa zenye kukidhi viwango.

erikali imekipongeza kiwanda cha vinywaji
baridi ya bonite ya moshi kwa kutekeleza kwa
vitendo usimamizi wa sheria katika uzalishaji wa
bidhaa zenye kukidhi viwango vinavyokubalika na
hifadhi ya mazingira bila kuathiri jamii
inayoizunguka kiwanda hicho.
Naibu waziri wa nchi,muungano na mazingira
Bw.Luhanga Mpina ametoa pongezi hizo wakati
alipotembelea kiwanda hicho na kujionea hali ya
uzalishaji wa bidhaa zake zikiwemo soda za aina
mbali mbali na maji.
Bw mpina amesema, pamoja na suala la kukidhi
viwango vya uzalishaji wa bidhaa hizo kiwanda
hicho pia kinazingatia suala la hifadhi ya
mazingira na kuwa mfano wa viwanda na
makampuni ambayo ameyataka kweda kujifunza
bonite.
Mratibu wa baraza la taifa la hifadhi na
usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya
kaskazini Dr.Menar Jangu amesema,kiwanda
hicho kila walipokitembelea hata kwa kushtukiza
walikuta kila idara ipo katika mazingira mazuri ya
uzalishaji wa bidhaa zake.
Meneja wa masoko na mauzo wa kiwanda hicho
kanda ya kaskazini Bw.Christopher Loiruk
amesema,Bonite tangu ianze uzalishaji wa bidhaa
zake imekuwa ikizalisha bidhaa zinazokidhi
viwango vya kimataifa mwaka hadi mwaka.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post