Mkuu wa wilaya ya Iringa leo azindua wiki ya mahakama kwa maandamano mjini Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa leo amezindua wiki ya
mahakama kwa maandamano mjini Iringa
yaliyoongozwa na brass band ya Magereza.
Akihutubia majaji pamoja na wananchi amesisitiza
uharaka wa kutoa HAKI. kesi nyingi zinachelewa
kuisha na wananchi wengi wamedhrumiwa haki
yao na huu ni uvunjwaji katiba.
Pia amesisitiza wakimama wasimamiwe haki zao.
Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya
mwanasheria mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini
kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika?
Wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi. Bila
haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo.
Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa
Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia
kutembelea magereza yote ili kubaini
waliocheleweshewa haki zao
About

Previous
Next Post »

Ads Inside Post