SERIKALI ITAENDELEA KUWAFUNGIA MAGETI WATUMISHI WAZEMBE: Mhe. Dkt.Hamisi Kigwangwalla

Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa
umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za
walipa kodi hususan wa kipatao cha chini na
wale maskinini
Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo
Dkt.Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya
tano inawataka watumishi wote nchini kufanya
kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha
uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia
watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowav umilia watumishi
wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti
na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka
watumishi wa umma wafanye kazi ya
kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,mtumishi
akizembea tutamtumbua majipu,akichelewa
tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na
kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi
tu”.
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka
kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza
ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm
zinatimizwa.
“hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale
penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya
mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi”
Hatahivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto
wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto
wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni
bure na hakuna michango yoyote.
“natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango
yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka
kuwaandikisha watoto shule kwani shule
zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo.
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa
umma kujipanga na kama watagundulika ni
majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina
kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post