Hayo yamejiri katika mkutano wa 7 wa bunge la
11 linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma
ambapo Mwenyekiti wa kikao cha leo Andrew
Chenge amelikumbusha bunge kuhusiana na kauli
aliyoitoa mbunge huyo tarehe 01/02/2016.
Mbunge huyo alisema kwamba Waziri Harrison
Mwakyembe alihusika kununua mabehewa feki
274 jambo ambalo lilizua mjadala mkali na bunge
kumtaka mbunge huyo atoe ushahidi ndani ya
siku 3.
Mwenyekiti Andrew chenge amesema kuwa
mbunge huyo alitakiwa kwa mujibu wa kanuni za
bunge kanuni ya 63(6) atoe ushahidi kwa ofisi ya
bunge na ndani ya siku zote ofisi ya bunge
haijapata ushahidi huo.
Kutokana na Mbunge huyo ambaye pia ni mke wa
aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini David
Kafulila NCCR Mageuzi kushindwa kutekeleza
maamuzi ya bunge mwenyekiti wa bunge
amemtaka kufuta kauli yake na mbunge huyo
akakaidi ndipo Mwenyekiti akamuamuru atoke nje
mara moja na kutohudhuria vikao vya bunge kwa
siku zilizobakia 2.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon