CHECKY: App Inayokujulisha Umetumia Simu Mara Ngapi Kwa Siku!

Checky inajibu swali dogo! Natumia simu
yangu mara ngapi kwa siku? Jibu ni mara
nyingi (ha!). Hii App inakuambia ni mara
ngapi umetumia simu kwa siku na pia inatoa
ramani ya sehemu ulizotumia simu hiyo. App
hii inasaidia sana kama mtu simu huwa
inakupotezea mda sana na unapenda punguza
matumizi.
Haipingiki kuwa kuna mambo mabaya katika
maisha yetu yanayosababishwa na teknolojia
hasa kwa teknolojia ile iliyopo upande wetu
kila saa: Simu-janja (SmartPhone) zetu. Ni
karne ya 21, huelewi kitu? unaangalia simu
yako, unataka jua kitu unaona aibu kuuliza?
unaangalia simu yako. Upo kwenye foleni?
Basi unatazama simu yako. Mtu kakuangalia
jicho baya? Haraka! Unaamia kwenye simu
yako kutwiti au kuandika Facebook kuhusu hilo
jambo.
“Kama Watu Wengi, Naipenda Sana Simu
Yangu” alisema mwanzilishi wa Calm, Alex
Tew
Labda nikuulize swali hivi ni mara ngapi
umetoa simu mfukoni kwa lengo la kuangalia
saa lakini ukajishangaa unafanya mambo
mengine? Ndio kabisa hii sio habari mpya
kwetu, tunajijua kabisa hatujiskii kawaidi bila
kuingiza mikoni kwenye mifuko na vipochi
vyetu ili kutoa na kuangalia simu zetu mara
kwa mara na hii imekua ni tabia.
Checky imetengenezwa na Calm lakini sio
bidhaa ambayo walitumia muda kuikuza.
Checky ni app rahisi sana na madhumuni yake
mengine ni kuleta kiki kwa kampuni, ambayo
imedhamiria kuingiza hela kupita App baadae.
CHECKY: Inakusaidia kufahamu tabia yako
ktk matumizi ya simu
Baada ya kujua taarifa jua ya matumizi ya
simu yako unaweza amua ku ‘share’ katika
mitandao ya kijamii. Kwa wale wenzangu
wenye tabia za kusahau simu zao, App hii
haitakua rafiki mzuri kwao. Hata hivyo simu
zinasababisha ajali, kutumia simu kidogo na
kwa mambo muhimu ndio mpango mzima!
Kushusha CHECKY bofya hapa iOs | Android

Previous
Next Post »

Ads Inside Post